Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 24 January 2018

TIMU MAALUM YA ADB YATEMBELEA TANZANIA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda (kulia) akiwa katika mazungumzo na Bw. Alieu Jeng, Mjumbe wa timu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank - ADB), walipomtembelea Wizarani tarehe 22 Januari, 2018. Timu hiyo yenye jumla ya wajumbe watatu ambao watakuwa nchini kwa lengo la kujadiliana na Serikali kuhusu maeneo ya vipaombele ambayo wanaweza kusaidia kupitia bajeti yao ya 2018/2019. Wakiwa nchini watakutana na Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali. Kwa mujibu wa wajumbe hao, bajeti hii itazingatia zaidi kusaidia Serikali kupitia maeneo ya vipaombele yaliyoanishwa ili kuwezesha sekta binafsi kuweza kuchochea uchumi wa nchi kupitia biashara na uwekezaji katika maeneo mbalimbali. Wajumbe hao waliwasili tarehe 14 Januari, 2018 na wanatarajiwa kuondoka tarehe 27 Januari, 2018. 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda (kulia), akiendelea na mazungumzo na wajumbe wa timu kutoka ADB ambao ni Bw. Alieu Jeng (Kushoto), Bw. Francois Nkulikiyimfura anayefuata na mwisho kushoto ni Bi. Eline Okuozeto. 
Katibu Mkuu, timu ya ADB na wataalam kutoka Wizarani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo.

No comments:

Post a Comment