Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday 24 December 2017

WAFANYAKAZI WA ZANTEL WASHIRIKI KUFANYA USAFI NA KUKABIDHI VIFAA KWA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA, ZANZIBAR.

Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha (kulia) akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dk. Msafiri Marijani mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi katika eneo la hospitali hiyo iliyopo Zanzibar hivi karibuni. Zantel ilikabidhi vifaa vyenye jumala ya thamani ya Sh.400, 000 hospitalini hapo.
Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dk. Msafiri Marijani (Mwenye fulana ya bluu) wakati wa zoezi la kufanya usafi na kukabidhi vifaa hospitalini hapo hivi karibuni mjini Zanzibar. Mkurugenzi huyo ambaye aliambatana na baadhi ya wafanyakazi wa Zantel alikabidhi vifaa vya usafi ikiwemo mifagio, ndoo na mafyekeo vyenye jumla ya thamani ya Sh. 400,000/= kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa usafi na kuzuia maambukizi kwa watu wanaofika hospitalini hapo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dk. Msafiri Marijani (Mwenye fulana ya bluu kushoto) akitoa neno la Shukrani kwa Mkuu wa Zantel, Zanzibar Mohamed Mussa Baucha (kulia) na wafanyakazi wote wa Zantel mara baada ya wafanyakazi hao kufanya usafi na kukabidhi vifaa vya usafi vyenye jumala ya thamani ya Sh.400,000 hospitalini hapo hivi karibuni mjini Zanzibar.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel wakishiriki kufanya usafi katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, zoezi ambalo lilifanyika hivi karibuni mjini Zanzibar. Tofauti na kufanya usafi, Zantel ilikabidhi vifaa vya usafi ikiwemo mifagio, ndoo na mafyekeo vyenye jumla ya thamani ya Sh. 400,000/= kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa usafi na kuzuia maambukizi kwa watu wanaofika hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment