Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 14 December 2017

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA NYUMBA 150 ZA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) ZILIZOPO IYUMBU, MKOANI DODOMA, DESEMBA 13, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge alipowasili katika sherehe ya ufunguzi wa nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Blandina Nyoni alipowasili katika sherehe ya ufunguzi wa nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017. 


Muonekano wa baadhi ya nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma zilizofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Desemba 13, 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)  Nehemia Mchechu akihutubia mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe ya ufunguzi wa nyumba 150 za NHC zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017. 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazai, Mhe. William Lukuvi akihutubia mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe ya ufunguzi wa nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Blandina Nyoni katika sherehe ya ufunguzi wa nyumba 150 za NHC zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika sherehe ya ufunguzi wa nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi kabla ya ufunguzi katika sherehe ya ufunguzi wa nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kitambaa kuashiria ufunguzi wa nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpa mkono wa pongezi mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ajira, Vijana, Kazi na Walemavu, Anthony Mavunde mara baada ya kufunua kitambaa kuashiria ufunguzi wa nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akijaribu kufungua bomba la maji katika moja ya nyumba aliyoingia kukagua mara baada ya kufungua nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia miundombinu ya chumbani katika moja ya nyumba aliyoingia kukagua mara baada ya kufungua nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Msanii Mrisho Mpoto na kundi lake pamoja na Msanii wa kikundi cha Mwanamila cha Dodoma mara baada ya kufungua nyumba 150 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu Manispaa ya Dodoma Desemba 13, 2017.
IKULU BLOG

No comments:

Post a Comment