Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 24 April 2017

TIGO, JACKSON GROUP KUSHIRIKIANA UZINDUZI WA KITABU APP

Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kitabu App ambayo iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania. Pembeni yake ni mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa.
Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa akielezea namna ya kupakua Kitabu App kwa watumiaji wa simu zenye mfumo wa Android uzinduzi wa Kitabu App ambayo iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania. Pembeni yake ni Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Chisel.
Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa akielezea namna ya matumizi ya Kitabu App kwa waandishi (Hawapo pichani) mara wakati wa uzinduzi wa Kitabu App ambayo iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania. katikati mtunzi wa hadithi Frank David na pembeni mwishoni ni Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael
Dar es Salaam - Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania hivi karibuni imeingia ubia na Kampuni ya Jackson Group kuzindua  App mpya ya mtandao  inayofahamika kama Kitabu App ambayo  iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania.

App hiyo  inaingia sokoni kama suluhisho sio tu kwa wasomaji  bali pia kwa waandishi wa vitabu  ambao sasa wanaweza   kuuza na kufuatilia na mauzo ya vitabu vyao  kupitia simu zao za mkononi, kwa kutumia mtandao wa Tigo 4G LTE ambao ni mkubwa, wa kasi na mpana nchini.

Kujumuisha  vitabu kwa njia ya sauti  katika jukwaa moja  inatarajiwa kuwa App hiyo itabadilisha jinsi ambavyo Watanzania watakavyojijengea mazoea kujisomea,  hali ambayo itakuwa ni kinyume na kupungua kwa mazoea hayo ambapo kwa kiwango kikubwa  kumekuwa kunahusishwa na  kuwepo kwa utamaduni mbovu wa kujisomea miongoni mwa wananchi.
     

Akizungumza wakati wa uzinduzi  wa App hiyo Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael alisema, “Kampuni yetu inaendelea  kuthibitisha  kujikita kwake katika kuwekeza n katika kuboresha utamaduni wa kujisomea nchini Tanzania. Tuna imani kwamba App hii  itahamasisha mvuto wa kujisomea  miongoni mwa jamii na hivyo kufufua  kudorora  kwa utamaduni  hapa nchini.”

Shisael alisema, “Tayari wateja wetu wengi  wanapenda kutumia simu kuchati na marafiki pamoja na wanafamilia,” na kuongeza, “Kupitia Kitabu App tunatoa jukwaa muhimu kwa waandishi, wachoraji na wasomaji kwa ujumla kufikia sehemu rahisi  ya kusoma mada mbalimbali kupitia simu ya mkononi. 

Akizungumzia kufurahia kwake  kushirikiana App  hiyo na wateja wa Tigo Shisael alibainisha kwamba  hivi sasa wanaweza kuvipata vitabu  wavipendavyo wakati wakifanya mambo mengine kwenye simu zao.

Akitoa maoni yake kuhusu App hiyo Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa  alisema, “App yetu ya Kitabu App ni ubunifu ulioendeshwa kimkakati  ukiwa unahamasishwa na kukua katika kujumuishwa kiteknolojia. Kupitia App hii tunawaruhusu waandishi wa vitabu kufikia kiwango cha hali ya juu cha usoamaji  kupitia simu zao za kisasa. Wakati tuna waandeishi wengi wenye vipaji katika  aina mbalimbali za vitabu, hali kadhalika kuna uhitaji mkubwa wa  uelewa ndani yake.”

Alisema, “Tunaamini kwa kuangalia  zaidi katika kukua kwa orodha yetu tunaweza kuleta mabadiliko ndani ya usambazaji kote nchini na kuirudisha tena furaha ya kujisomea  kwa Watanznania.”

Twissa aliongeza, “ Kitabu ni App  ya kuelimisha, kuburudisha  na kuunganisha na mada za kidini. Elimu  ni moja ya mitazamo yetu ya msingi, hivyo tunajenga ushirikiano  na tunatoa wito kwa taasisi za kielimu  kupakua mada zao, kuhifadhi kwa ajili ya kuchapisha na kusambaza vitabu.”

App ya Kitabu App inaweza kupakuliwa bure  na kwa hivi sasa  inapatikana katika simu za Android  ambapo mtumiaji  anatakiwa  tu  kutoa malipo kupitia TigoPesa kwa mada zinazohitajijka na mtu  binafsi.


No comments:

Post a Comment