Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 13 March 2017

MAXCOM AFRICA (MAXMALIPO) YAWAKARIBISHA WATANZANIA KUSHIRIKI UNUNUZI WA HISA KWA NJIA YA MTANDAO

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu wa Kampuni hiyo, Deogratius Lazari Mosha.

Kampuni ya Maxcom Africa (Maxmalipo) inawakaribisha watanzania kushiriki manunuzi ya hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye Soko la hisa la Dar es salaam(DSE) kwa njia ya mtandao (simu za kiganjani) na kufanya malipo kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo waliopo nchi nzima Tanzania.

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu wa Kampuni hiyo, Deogratius Lazari Mosha, amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kwamba Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kutumia mfumo madhubuti wa simu za viganjani unamwezesha Mtanzania kuweza kushiriki kwenye Manunuzi ya hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la awali la mitaji (primary markets ) kwa kupiga *150*36#, ameongeza kwamba baadhi ya makampuni hayo kwa sasa ni Vodacom na TCCIA.


Akifafanua hili, Lazari amesema ili Mtanzania aweze kushiriki Manunuzi ya hisa kwa mfumo huu anatakiwa kubonyeza *150*36# kisha ataingia kwenye Menyu ya soko la hisa na Kuchagua IPO kisha atachagua kampuni anayotaka kununua hisa, baada ya kufanya hivyo mteja atalazimika kujisajili na kisha atapata nafasi ya kuainisha idadi ya hisa anazohitaji(zisizo pungua 100 katika awamu ya kwanza).
Lazari ameongeza kwamba baada ya hatua ya uanishaji wa hisa, mteja atapokea ujumbe mfupi wa simu kutoka DSE wenye nambari ya kumbukumbu ya malipo, idadi ya hisa na kiasi anachotakiwa kulipia. Ili kukamilisha malipo haya mteja atatakiwa kufika kwa wakala yeyote wa Maxmalipo aliye karibu naye na kufanya malipo kama ilivyo ainishwa kwenye ujumbe aliopokea kwenye simu yake. Mteja anahimizwa kuhakikisha kwamba anapatiwa risiti pindi anapolipia hisa kwa mawakala wa Maxmalipo ili kutunza kumbu kumbu zake.

Kwa kuongezea, Lazari ameeleza kwamba mfumo huu rafiki unamwezesha mteja kushiriki manunuzi ya hisa kadiri ya uwezo wake (Mfano, Mteja Anaweza kila siku akanunua hisa 100 kulingana na kipato chake au zaidi). Pamoja na mwakala wa Maxmalipo mteja anaweza kulipia kwa kutumia mitandao ya simu.

Mfumo huu wa kununua hisa kwa simu za kiganjani ( *150*36#) umetengenezwa na kampuni ya kitanzania ya Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na Soko la hisa la Dar es Salaam(DSE) na ni mfumo rasmi wa kuuza na kununua hisa kwenye soko la hisa.

Watanzania wamepewa wito wa kushiriki ununuzi wa hisa kwa njia ya simu ya kiganjani na kuhakikisha wanafanya malipo mapema kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo walioko nchi nzima takribani Mawakala Elfu kumi na sita .

No comments:

Post a Comment