Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 20 January 2017

TIMIZA MALENGO NA NDOTO ZAKO KUPITIA ‘BONUS ACCOUNT’ YA NMB


Unafahamu kwamba ni rahisi kufikia malengo yako ya kujiwekea akiba ukiwa na “NMB Bonus Account au Business Savings Account” ambayo inakupa faida hadi 13%? Mfano, ukiwa na lengo la kujiwekea akiba ya shilingi 500,000 kwa mwaka 2017 inabidi uweke kiasi cha shilingi 42,000 tu kwa mwezi na ukiwa na nidhamu ya kuhakikisha kwamba kiwango hakipungui kiasi ulichojiwekea basi utakuwa umechagua njia sahihi kuelekea kutimiza ndoto zako. Jambo la msingi ni kuhakikisha unakuwa na akaunti ambayo haiingiliani na matumizi yako ya kila siku, hii ni hatua muhimu katika kutimiza malengo binafsi uliyojiwekea ama ya kibiashara.

NMB inatambua umuhimu wa kujijengea nidhamu ya kuweka akiba na kuwaletea wateja wake bidhaa zitakazowasaidia kuweka akiba na pia kuhakikisha wanakuza na kupata maendeleo binafsi na ya kibiashara. 



‘Bonus Account’ na ‘Business Savings Account’ ni akaunti maalum kwa ajili ya wateja wanaotaka kutimiza malengo yao binafsi au ya kibiashara. Labda ungependa kuweka akiba kwa ajili ya kulipia ada ya mwanao mwakani, kununua nyumba miaka minne ijayo au kuanzisha biashara miaka siku za usoni, ukiwa na akaunti hizi utakuwa umepata njia sahihi ya kufikia malengo yako.

Wasiliana na NMB leo kupitia namba 0800 002 002 utimize matarajio yako kupitia NMB Bonus Account na NMB Business Savings Account.

No comments:

Post a Comment