Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 31 August 2016

SAFARI LAGER YAZINDUA UJAZO MPYA WA BIA


Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) imezindua ujazo mpya wa bia ya Safari Lager kwa lengo la kuleta urahisi na unafuu kwa wanywaji wa bia hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi maalumu uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa bia hiyo, Edith Nasuwa alisema, "Safari Lager imekuwa bia ya kwanza ya kitanzania kuzindua kopo kubwa lenye ujazo wa mililita 500 hapa Tanzania". Kopo hili limezinduliwa mahususi ili kuendana na wakati na kumpa mnywaji urahisi pale anapotaka kuburudika na kinywaji hiki baada ya kazi.”

Amesisitiza kwamba hakuna mabadiliko yoyote kwenye ladha ya Safari Lager ila kilichobadilika ni muonekano wa kifungashio tu.

Kwa sasa, Safari Lager ya kopo inapatikana katika mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema Safari Lager inatambua kuwa muda na fedha ni jambo la thamani kwa wateja na ndicho kinachowahamasisha kuendelea kubuni njia za kukidhi mahitaji ya wateja wao.

No comments:

Post a Comment