Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 5 February 2016

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MALENGO

Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi kampeni ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na kulia ni Meneja wa kampeni hiyo, Mtenya Cheya.
Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki ya NBC, Mussa Jallow (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza cha benki hiyo, Andrew Massawe.
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza cha benki hiyo, Andrew Massawe (kushoto), akizungumza kuhusu faida mbalimbali za mteja wa benki hiyo atakayeshiriki kampeni ya malengo ya NBC. Kulia ni Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki hiyo, Mussa Jallow.
Kampeni ya malengo itadumu kwa muda wa miezi mitatu kutoka Februari 4 mpaka Aprili 30 2016. Katika kipindi hicho cha miezi mitatu ya kampeni, wateja wanaoweka fedha watafaidika na kiwango cha kuvutia cha riba na kuwa katika nafasi kubwa ya kushinda gari mpya aina ya Toyota Land Cruiser Prado kama linavooeneka pichani.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NBC wakipozi kwa picha wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam. Hii ni kampeni ya tatu ya kuwekeza kuzinduliwa na NBC na kama ilivyo katika miaka mingi kampeni zote zimekuwa za mafanikio makubwa katika suala zima la mrejesho na ufahamu wa wateja. Mwaka jana NBC ilizindua kampeni ya kuwekeza iliyopewa jina la “Weka Upewe” ambayo ilishuhudia NBC ikitoa zawadi kadhaa kwa wateja wao nchini kote.

No comments:

Post a Comment