Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 30 April 2015

TANZANIANS PARTICIPATE IN THE MANAGEMENT OF NATURAL GAS REVENUE

Deputy Minister of Communication, Science and Technology, January Makamba sits on an expert panel to answer questions from the respondents.
Press Conference with Aidan Eyakuze from TWAWEZA (first left), Innocent Bash from TEITI (second left), Dr. Abel Kinyondo from REPOA (third left), Mujobu Moyo from CDG (second right) and Silas Olang from NRGI (first right).
Dr Abel Kinyondo, Economist & Senior Researcher at REPOA giving his opening remarks at the conference which took place at Blue Pearl Hotel in Dar es Salaam recently.

BENKI YA POSTA YAJIVUNIA UTENDAJI BORA KWA MWAKA 2014 ULIYOIPA FAIDA NONO

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Kitewita Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Pamoja nae ni Mkurugenzi Fedha, Regina Samakafu (katikati) na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda Ngongi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi wakati wa kutangaza utendaji wa benki hiyo kwa mwaka 2014 ambapo TBP walipata faida ya shilingi 10.28 bilioni kabla ya kodi. Katikati ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa benki hiyo, Peter Mapigano na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Teknolojia, Jema Msuya.
Mkurugenzi wa Mipango wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Bernadethe Joseph Gogadi (kushoto) akifuatilia mkutano huo ambapo waandishi wa habari nao walikuwepo kuchukua taarifa kama wanavyoonekana pichani.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI UNAOENDELEA JUU YA SARAFU YA SH. 500/=


Asilimia 94 ya madini katika sarafu ya sh. 500 ni chuma na asilimia 6 ni Nickel, ameeleza Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki katika Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Marcian Kobello. 

Pia ndivyo ilivyoelezwa wakati wa uzinduzi wa sarafu hii mnamo mwezi Septemba mwaka jana kabla haijaingizwa katika mzunguko mwezi Oktoba 2014. 

Bw. Kobello amesema hadi sasa sarafu zenye thamani ya sh. 1,162,000,000/- zimekwishasambazwa kote nchini na kwamba kuna kiasi cha kutosha cha sarafu hiyo endapo itahitajika.

“Hakuna kabisa madini ya fedha katika sarafu ya sh. 500,” amesema Bw. Kobello na kuongeza kuwa haitegemewi kwamba mfanyabiashara yeyote anaweza kununua sarafu hiyo kwa bei ya juu kuliko thamani yake halisi.

“Kwa hiyo, tunapenda kuwafahamisha wananchi kwamba kuna kiasi cha kutosha cha sarafu za sh. 500 nchini na kwamba kununua sarafu hiyo kwa bei ya juu kuliko thamani yake ni kujiingizia hasara,” ameeleza mkurugenzi huyo.

Pia ameongeza kuwa Nickel sio miongoni mwa madini maarufu kwa ajili ya kutengeneza vidani vya thamani.

Imetolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
Aprili 29, 2015.


EXIM BANK KEEN ON SUPPORTING THE GOVERNMENT ANTI-MALARIA CAMPAIGNS

Exim Bank Arusha Seniour Branch Manager, Mr. Fredrick Umiro (right) hands over treated mosquito nets to Surgeon Mr. Zubera Mtengwa (second left) of Mount Meru Hospistal in Arusha. The nets were donated by the bank as part of its Corporate Social Responsibility (CSR) activities to mark the World Malaria Day which was marked on April 25th this year. Witnessing are the bank’s Sales Manager, Mr. Assed Ali Naqvi (left) and other representatives of Mt. Meru Hospital.
Ligula Hospital Chief Medical Officer, Dr. Mohamed Gwao (second right) together with Exim Bank Mtwara Customer Service and Operations Manager, Mr Chande S. Chande (right) display the treated mosquito nets handed over by the bank to the Mtwara’s regional hospital recently during the World Malaria Day which was marked on 25th of April. The donation is part of the bank’s Corporate Social Responsibility (CSR) activities, aimed at supporting the government campaigns against Malaria. Witnessing are the representatives from the bank and Ligula hospital.

BENKI YA NMB YAFUNGUA RASMI TAWI LA SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mh. Dk. Perseko Vincent Kone (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la Singida, kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati Bw. Ole Loibanguti na Meneja wa NMB tawi la Singida, Bi. Christine Mwangoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mh. Dk. Perseko Vincent Kone akipata maelezo kuhusu huduma na bidhaa zinazo tolewa katika tawi hilo kutoka kwa Meneja wa NMB tawi la Singida, Bi. Christine Mwangoma.
Benki ya NMB imefungua rasmi tawi lake jipya la Singida. Tawi hilo litakuwa na huduma zote za kibenki kama yalivyo matawi mengine ya NMB nchini kote. Tawi hili limefunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mh. Dk. Perseko Vincent Kone.

Kufunguliwa kwa tawi la Singida sasa kutaharakisha maendeleo ya wakazi wa Mkoa wa Singida na pia kurahisisha biashara kati ya wananchi wa mji huo na wa maeneo ya jirani.

COVENANT BANK YAWAITA TFF, YAJITOLEA KUWADHAMINI TWIGA STARS

Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa klabu ya Mpira ya Lucenti, itakayoshiriki michuano ya kanda ya Nyanda za juu kusini, itakayofanyika Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kushoto ni Meneja Fedha wa Benki hiyo Patrick Kyamba na Mwenyekiti wa Klabu ya Lucent, Yusuph Liambe.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, (Katikati) Mwenyekiti wa Klabu ya Lucenti, Yusuph Liambe, Mkurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo Margreth Kyarwenda wakiwa wameshikilia vifaa vya michezo vilivyotolewa na Covenant Bank kwa timu hiyo itakayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za juu kusini itakayofanyika Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja akimkabidhi Mwenyekiti wa Klabu ya Lucenti, Yusuph Liambe vifaa vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya Timu hiyo itakayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za juu kusini itakayofanyika Sumbawanga Mkoani Rukwa. Wanaoshuhudia ni Meneja Fedha wa benki hiyo. Patrick Kyamba na Mkurugenzi wa Bodi Margreth Kyarwenda.
Dar es Salaam, 28 Aprili 2015 - Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank Sabetha mwambenja, amewaita viongozi wa Soka Nchini TFF, kwenda kujadili namna ambavyo benki hiyo inaweza kuisaidia Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars ambayo imefuzu kushiriki Michuano ya All African Games itakayo fanyika nchini Congo mwezi septemba.

Hayo yametanabaishwa na Mkurugenzi huyo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Lucenti inayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za juu kusini yatakayo fanyika Sumbawanga baada ya kufudhu michezo ya ligi dalaja la tatu baada ya kuulizwa swali na waandishi waliotaka kujua ni namna gani benki hiyo inaweza kuisaidia timu hiyo ya Taifa inayosuasua katika maandalizi.

NHC NA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM ZATILIANA SAINI MKATABA WA MANUNUZI YA ENEO LA OFISI JENGO LA MOROCCO SQUARE

Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. (Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii).
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini wiki iliyopita.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini wiki iliyopita.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudua NHC na DSE wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudua NHC na DSE wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.
Watendaji wa NHC na DSE wakibadilishana mawazo wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa Tuntufye Mwambusi na Meneja wa Uendelezaji Biashara wa NHC, Willia Genya wakibadiliashana mawazo katika hafla hiyo.

Wednesday 29 April 2015

BILIONEA ALIKO DANGOTE AKAGUA UFUKWE ATAKAOJENGA BANDARI YAKE YA KISASA MTWARA

Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti wiki iliyopita.
Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dangote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute. (PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Alhaji Dangote akipata maelezo kuhusu eneo alilopewa na Serikali ya Kijiji cha Mgao lenye ukubwa wa heka 2500 sawa na hekta 1000. Anatarajia kuanza kujenga bandari hiyo mwaka huu.
Ndege iliyomleta Dangote ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara tayari kwenda kukagua eneo atakapojenga bandari yake.
Dangote akilakiwa na Esther Baruti.
Alhaji Dangote akilakiwa na Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Majanbu.

TIGO LAUNCHES BID TO BECOME BIGGEST 4G NETWORK IN TANZANIA


Dar es Salaam, 24th April 2015.
TIGO Tanzania has launched a brand new 4G LTE technology that will make it the biggest and fastest Internet network in the country.

Speaking at the launch, Tigo Interim General Manager Cecile Tiano said: “This once again demonstrates our company’s commitment to the digital lifestyle transformation and its leadership in delivering cutting edge technology and innovation in this market.”

The 4G LTE network means faster speeds to surf and download content from the Internet and make Skype calls. It also significantly enhances the customer experience for video streaming or conferencing. The new technology is about 5 times faster than the 3G technology currently available in the market.

The 4G LTE technology is a standard for wireless communication of high-speed data. It has the capacity to efficiently transfer large amounts of data at an unparalleled speed. It can also accommodate more applications such as video conferencing, high definition content, video blogs, interactive games and video downloads on social networking sites.

With the surging use of smartphones among the Tanzania population, 4G technology will enable Tigo customers to enjoy a world class experience of increased speed and quality of internet access through the network.

“Today’s launch covers Masaki and Mlimani City areas within Dar es Salaam but our plan is to fully cover the city by end of July, ensuring quality coverage in Kinondoni, Ilala and Temeke in places such as Upanga, Posta, Tegeta, Mbagala, Tabata, Kimara, Mbezi, Ukonga, Salasala, Mikocheni, Msasani, Sinza and so on,” Ms Tiano explained.

“We will also launch 4G in Arusha, Dodoma, Morogoro, Moshi, Mwanza and Tanga by end of August. This will make us by far the biggest 4G network in Tanzania,” she added.

The 4G technology launch is part of Tigo’s commitment to continue improving the quality and coverage of its network and bring world class products and services to Tanzanians.

Tigo recently announced plans to invest US $120 million in 2015 on its network expansion and improvement. The investment includes scaling up its 3G sites and fibre network countrywide to make the internet accessible to more users.

FACT BOX

Tigo new 4G technology makes Tigo the fastest Internet network in the country

The company is investing $ 120 million on network improvement and expansion in 2015

Network has 8.5 million total subscribers

4G will increase internet speed by 5 times from the current 3G technology

4G launch covers Masaki, Mlimani city areas in Dar

4G to cover whole city and six regional capitals by August 2015

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA CEO WA STANDARD CHARTERED TANZANIA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini Bi. Liz Lloyd alipomtembelea Wizarani kwa ajili ya mazungumzo na Mhe. Maalim.
Mhe. Maalim akimtambulisha kwa Bi. Lloyd Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya.
Mhe. Dkt. Maalim akizungumza na Bi. Lloyd.
Ujumbe alioambatana nao Bi. Lloyd wakifuatilia mazungumzo.
Bi. Lloyd nae alipata wasaa wa kuchangia hoja wakati wa mazungumzo na Dkt. Maalim.
Balozi Yahya (kushoto) akiwa na Katibu wa Naibu Waziri Bw. Adam Isara wakisikiliza mazungumzo kati ya Dkt. Maalim na Bi. Lloyd (hawapo pichani).
Mazungumzo yakiendelea.

Tuesday 28 April 2015

BANK OF AFRICA TANZANIA, YAZINDUA UCHANGIAJI MATIBABU KWA WATOTO WALIOPINDA MIGUU

Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa matibabu ya watoto 400 wenye matatizo ya kupinda miguu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kusaidia matibabu ya watoto 400 wenye matatizo ya kupinda miguu. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya kupinda miguu katika mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akionyesha picha za watoto wenye matatizo ya kupinda miguu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kusaidia matibabu ya watoto 400 wenye matatizo yakupinda miguu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akionyesha picha za watoto wenye matatizo ya kupinda miguu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia Hospitali ya CCBRT katika mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa huo.

BENKI YA NMB YAPATA TUZO KWA KUCHANGIA ZAIDI HUDUMA ZA JAMII

Afisa Mtendaji Mkuu Mtarajiwa wa Benki ya NMB, Bi Ineke Bussermaker akipokea tuzo ya Mshindi wa jumla kama taasisi inayochangia zaidi huduma za jamii kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdala Kigoda.
Afisa Mtendaji Mkuu Mtarajiwa wa Benki ya NMB, Bi Ineke Bussermaker pamoja na Waziri wa Viwanda, Dk. Abdala Kigoda wakipata picha baada ya makabidhiano ya tuzo hiyo.
Benki ya NMB imeibuka mshindi wa kwanza na wa jumla katika makampuni ya biashara yanayojali zaidi jamii kwa kutoa sehemu kubwa ya faida yake kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii ya kitanzania.

Ushindi huo umetokana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya utafiti wa huduma za maendeleo ya jamii, Research Centre for Social Development Services kwa kushirikiana na kampuni mwenza ya Konsalt Limited imetoa tuzo hiyo kwa NMB baada ya kujiridhisha kuwa ndiyo benki inayoongoza kwa kusaidia jamii zaidi.

RAIA WATATU WA KIGENI WAKAMATWA KWA MAKOSA YA WIZI WA MTANDAO KATIKA MABENKI JIJINI DAR ES SALAAM

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa watatu raia wa kigeni kwa makosa yanayohusiana na wizi wa mtandao kwa lengo la kuiba katika vyombo vya fedha kama mabenki, maduka ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) au kuingilia miamala ya fedha zinazosafirishwa na wateja kutoka nje na ndani ya nchi.

Polisi wa kikosi Maalum cha kupambana na wizi wa mtandao (Cyber Crime) walipata taarifa za kuaminika kwamba watu hao watatu walikuwa katika mazingira ya kutiliwa mashaka na ndipo Polisi walienda Mtaa wa Mindu eneo la Upanga na kuwakamata. Watu hao walikutwa katika nyumba namba 416 iliyopo katika ghorofa ya nne na walitambuliwa kwa majina yafuatayo:

1. FOTIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Raia wa nchini UGIRIKI mwenye Passport namba AK2669977.

2. ATHANASIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Mkazi wa Ugiriki mwenye Passport namba AK3049876.

3. PANAGIOTIS S/O ANGELIDIS, Miaka 25, Mkazi wa Upanga, Raia wa UGIRIKI mwenye Passport namba AK2644930.

Watu hao watatu ambao ni raia wa nchini Ugiriki kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba wamekuwa wakiingia na kutoka nchini Tanzania na kwenda nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya katika namna ambayo inaonyesha kuwa ni wahalifu wa kimataifa kupitia mitandao.

BALOZI KAMALA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA BIASHARA UBELIGIJI

Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Laxembourg na Jumuiya ya Ulaya, Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa kwanza kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka nchi mbalimbali duniani baada ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Biashara la Kimataifa linalofanyika Genval, Ubeligiji.

Makampuni zaidi ya 500 yakiwemo 50 kutoka Tanzania yanashiriki Kongamano hilo.

Makampuni hapo yanatoka nchi zinazozungumza kifaransa. Tanzania ni nchi pekee inayozungumza kingereza iliyokaribishwa kushiriki. Kesho, Balozi Kamala atawasilisha mada ya kubainisha fursa za uwekezaji na biashara zinazopatikana Tanzania. 



NBC LAUNCHES E-STATEMENT SERVICES

Musa Jallow, NBC Head of Retail Banking.

HELLOFOOD TANZANIA LAUNCHES A NEW WEBSITE

Hellofood an online food delivery company and its affiliated brands Foodpanda and Delivery Club have launched a newly redesigned website that caters more for customer needs. The website is created with customer experience firmly in mind.The new design aims to provide a faultless user experience and showcases its wide range of restaurants in an attractive and visual way.

Some key features of the website include a cleaner and more attractive design, with restaurants arranged in a friendlier manner. The website allows for a more engaging user experience with enhanced search and navigation.It lets the customer search for restaurants easily and quicker than before. The new feature allows users to log into the hellofood app using a customer’s facebook account.

Joe Falter, founder and CEO of Hellofood Africa had this to say about the new website “Our brand new website marks another massive product milestone for hellofood, and takes us one step further towards our goal of offering amazing variety and seamless ordering with customer experience at the core”.

WAZIRI NYALANDU AKAGUA VIFAA MBALIMBALI VILIVYONUNULIWA NA TAASISI YA BUFFET FOUNDATION MJINI MWANZA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikagua gwaride la heshima jana alipowasili Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya kompyuta maalum zinazotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijaribu moja ya darubini zinazotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini