Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 29 April 2015

BILIONEA ALIKO DANGOTE AKAGUA UFUKWE ATAKAOJENGA BANDARI YAKE YA KISASA MTWARA

Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti wiki iliyopita.
Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dangote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute. (PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Alhaji Dangote akipata maelezo kuhusu eneo alilopewa na Serikali ya Kijiji cha Mgao lenye ukubwa wa heka 2500 sawa na hekta 1000. Anatarajia kuanza kujenga bandari hiyo mwaka huu.
Ndege iliyomleta Dangote ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara tayari kwenda kukagua eneo atakapojenga bandari yake.
Dangote akilakiwa na Esther Baruti.
Alhaji Dangote akilakiwa na Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Majanbu.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akisalimiana na Alhaji Dangote.
Alhaji Dangote akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (kushoto) Mwakilishi wake hapa nchini, Esther Baruti na Balozi Dk. Majanbu.
Alhaji Dangote akizungumza na Esther Baruti.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dedengu akimtambulisha Alhaji Dangote kwa wananchi alipowasili katika Kijiji cha Mgao, ambapo amepewa Dangote eneo la ujenzi wa Bandari.
Alhaji Dangote akisaini katika kitabu cha wageni alipowasili katika Kijiji cha Mgfao kukagua eneo la ujenzi wa Bandari pamoja na kiwanja alichopewa na wanakijiji kujenga makazi yake. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Abdulrahman Shaa
Wananchi wakiangalia msafara wa Alhaji Dangote uliokuwa unakwenda eneo ambapo bandari itajengwa.
Alhaji Dangote akiwa na viongozi wa Kijiji cha Mgao pamoja na wananchi akikagua uwanja heka mbili na nusu aliyopewa kwa ajili ya kujenga makazi yake katika kijiji hicho.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa makazi yake. Kijiji nacho kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine ya maendeleo.
Msafara wa Alhaji Dangote ukielekea eneo patakapojengwa Bandari.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa akihojiwa na wananchi kuhusu manufaa watakayopata wanakijiji endapo Badari hiyo ikijengwa.
 Alhaji Dangote akizungumza na wanahabari kuhusu ujenzi wa bandari hiyo.

Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa.





Alhaji akijadiliana jambo na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha saruji, Kushoto ni Paschasia Ngaiza Mama Mzazi wa Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais wa Tanzania, Premy Kibanga ambaye pia alikuwepo kwenye ziara hiyo.
Alhaji Dangote akizungumza na Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Majanbu muda mfupi kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akimuaga Alhaji Dangote uwanjani hapo.
Alhaji Dangote akiteta jambo na mwakilishi wake hapa nchini, Esther muda mfupi kabla ya kupanda ndege kwenda Ethiopia na hatimaye Lagos, Nigeria.
 Alhaji Dangote akiaga.
Dedengu akijadiliana jambo na Esther.
Balozi wa Nigeria nchini, akizungumza jambo na Dendengu pamoja na Esther. Kulia ni Paschasia Ngaiza.
Ndege iliyombeba Alhaji Dangote na ujumbe wake ikiondoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara.

No comments:

Post a Comment