Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 26 November 2014

WIZARA YA UJENZI KUJENGA DARAJA JIPYA LITAKALOPITA BAHARINI PEMBEZONI MWA DARAJA SELANDER

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionyesha sehemu ambazo daraja hilo jipya litakapojengwa pembezoni mwa daraja Selander kuanzia hospitali ya Aghakan hadi barabara ya Kenyatta. Sehemu ya Daraja hilo pekee litakuwa na urefu wa km 1.03.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiwa na ujumbe kutoka Serikali ya Korea Kusini pamoja na Wizara ya Ujenzi mara baada ya kusaini Mkataba wa Muhtasari wa Majadiliano hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akimshukuru Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli mara baada ya hafla ya utiaji sahihi wa Muhtasari wa Majadiliano.
Tukio la utiaji sahihi likiendelea kama inavyoonekana pichani.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Eng. Patrick Mfugale akionyesha mchoro wa nguzo kubwa za daraja hilo zitakazopita baharini pembezoni mwa daraja la Selander huku Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe wakifatilia kwa makini.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akifafanua kuhusu ujenzi wa daraja hilo. Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU) Wizara ya Ujenzi.

No comments:

Post a Comment