Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 31 October 2014

NMB YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA WEKA NA USHINDE

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Salie Mlay akimkabidhi Bi. Florance Kasenene Mshindi wa Bajaj katika tawi la NMB Sinza. Akishuhudia ni Meneja wa NMB tawi la Bank House - Bw. Leon Ngowi.

Washindi wa zawadi za Weka na Ushinde wakifurahia zawadi zao baada ya kukabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Kati Bw. Ole Loibanguti (tatu kushoto)i katika hafla iliyofanyika katika tawi la NMB Dodoma.

Bw. Genenis Mbaga akiwa ndani ya bajaj yake aliyokabidhiwa katika tawi la NMB Same baada ya kuibuka mshindi wa Weka na Ushinde promosheni.

BENKI ya NMB juzi ilikabidhii zawadi kwa washindi wa promosheni ya Weka na Ushinde. Zaidi ya wateja 165 walijishindia zawadi mbali mbali ikiwa ni: washindi 17 wa Bajaj, wa Pikipiki aina ya 'Boxer' 16 na Baiskeli aina ya 'Phoenix' 137.

Washindi hao wamepatikana ndani ya mwezi mmoja tangu kuanzishwa kwa promosheni hii ya Weka na Ushinde ambayo inaendelea hadi mwishoni mwa mwaka huu 2014.

Benki ya NMB inatoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuchangamkia fursa kwa kushiriki kampeni ya Weka na Ushinde ambayo itawawezesha kushinda zawadi zenye thamani zaidi ya milioni 500. Unachotakiwa kufanya ni kuweka kiwango cha fedha kisichopungua shilingi elfu hamsini kwenye akaunti yako kila wiki na kujiongezea nafasi zaidi ya kushinda.

No comments:

Post a Comment