Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 30 September 2014

KUNDI LA ORIJINO KOMEDY WAJIUNGA NA HUDUMA YA BIMA ITOLEWAYO NA CRDB MICROFINANCE INSURANCE BROKERS

Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers, Arthur Mosha (kushoto) akimkabidhi Kadi ya huduma ya bima ya maisha, mazishi na ulemavu wa kudumu Kiongoni Mkuu wa Orijino Komedy Company, Sekioni David (kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ofisi za CRDB Mikocheni jijini Dar.

Msanii Lucas Mhuvile ‘Joti’ akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers, Arthur Mosha.

Msanii Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ (kulia) akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers, Arthur Mosha. Wa pili kulia ni Meneja Mkuu wa African Life Assurance, Nura Masoud na Kushoto ni Meneja Mkuu wa AAR Insurance, Majala Manyama.


Meneja Uhusiano wa CRDB Microfinance Insurance Brokers, Nargis Mohamed (kulia) akiwa na Msanii wa Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company, Mjuni Silvery ‘Mpoki’ katika hafla hiyo.

Picha ya pamoja.

CRDB Microfinance Insurance Brokers ambao ni wakala wa bima za aina zote ikiwemo bima ya afya, moto, nyumba na maisha wakishirikiana na kampuni zaidi ya kumi za bima nchini Tanzania, wamefanikiwa kuwapatia huduma ya bima ya maisha, mazishi na ulemavu wa kudumu Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company wao na familia zao kupitia African life Assurance (Tanzania) Ltd na bima ya afya wao na familia zao kupitia Kampuni ya AAR Insurance Tanzania.

CRDB Microfinance wanayo furaha kubwa kwa kuwapatia wasani hao huduma hiyo, kwani siku zote imekuwa ikifahamika kuwa msanii ni kioo cha jamii. Wasanii hao waliofanikiwa kujiunga na huduma hizo ni pamoja na Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Alex Chalamila ‘McRegan’ na Kiongozi wa kundi hilo, Sekioni David na wengine ni Herry pamoja na Jonas.

Huduma hii inawahamasisha wasanii wengine, wanahabari, wanamitindo na watanzania wote wa hali zote kutembelea ilipo CRDB Bank tawi lolote nchini Tanzania, ili waweze kupata huduma nzuri ya na haraka ya bima "ndani ya mikono salama".

Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment